59 episodes

Inahusu masuala ya ujasiriamali, biashara ndogo ndogo, ushauri kuhusu uwekezaji na shughuli nyinginezo za kiuchumi.

Uchumi na Biashara Standard Media

    • Arts

Inahusu masuala ya ujasiriamali, biashara ndogo ndogo, ushauri kuhusu uwekezaji na shughuli nyinginezo za kiuchumi.

    Mbona Magari ya Umeme? | Uchumi na Biashara Podcast

    Mbona Magari ya Umeme? | Uchumi na Biashara Podcast

    Baadhi ya kampuni za uagizaji na uuzaji wa magari nchini zimebadili mwelekeo na sasa zinajitosa katika uagizaji wa magari yanayotumia umeme. Kampuni ya hivi punde kufanya hivyo ni ya BasiGo na ya kwanza kuagiza mabasi 15 ya umeme ambayo yalitengenezwa na Kampuni ya BYD Automotive iliyo nchini Uchina. Mabasi haya tayari yamewasili nchini kupitia Bandari ya Mombasa na yanatarajiwa kutoa huduma za uchukuzi jijini Nairobi. Lakini je, mbona wafanyabiashara waanze kufuata muelekeo wa uagizaji wa magari ya umeme? Robert Menza amewahoji baadhi ya washikadau katika sekta hiyo

    • 14 min
    Kuvuma kwa Utalii Krisimasi na Mwaka Mpya | Uchumi na Biashara Podcast

    Kuvuma kwa Utalii Krisimasi na Mwaka Mpya | Uchumi na Biashara Podcast

    Huku msimu wa Krimasi na Mwaka Mpya ukikaribia Sekta ya Utalii inategemea sana msimu huu kuimarika kutokana na watalii wa mataifa ya kigeni wanaolenga kuzuru maeneo mbalimbali ya kitalii nchini. Mojawapo ya maeneo hayo ni eneo la Pwani hususani Kaunti ya Mombasa. Je, wafanyabiashara hasa wa hoteli za kitalii wamejiandaa vipi msimu huu? Robert Menza amezungumza na Josephat Iha ambaye ni Meneja wa Mauzo katika Mkahawa wa Massai Beach.

    • 21 min
    Serikali saidia, biashara zetu zazorota | Uchumi na Biashara Podcast

    Serikali saidia, biashara zetu zazorota | Uchumi na Biashara Podcast

    Licha ya serkali kuahidi kushughulikia changamoto za wafanyabiashara wadogo wadogo, bado mahangaiko yanashuhudiwa mwezi mmoja baada ya Kenya Kwanza kuchukua hatamu za uongozi. Wengi wa wafanyabiashara hao wanalalamikia kuongezwa kwa bei ya mafuta, na kusababisha hasara katika sekta ya matatu. Charles Macharia, mhudumu wa teksi na Jimmy Mwangi, mhudumu wa matatu wanatishia kugura biashara hii.
    Mwanahabari wetu Edwin Mbugua amefanya mazungumzo na baadhi ya wafanyabiashara hao katika Kaunti ya Nyeri.

    • 14 min
    Nyumba za Bei Nafuu | Uchumi na Biashara Podcast

    Nyumba za Bei Nafuu | Uchumi na Biashara Podcast

    Washikadau mbalimbali wanaunga mkono mpango wa ujenzi wa nyumba kwa bei nafuu unaoendelezwa na serikali, mfano mradi wa Buxton Point katika Kaunti ya Mombasa unaoendelezwa na mfanyabiashara, Suleiman Shahbal na Serikali ya Kaunti ya Mombasa. Robert Menza amezungumza na Martin Kariuki, anayesimamia uuzaji wa nyumba hizo.

    • 18 min
    Uzalishaji wa mayai | Uchumi na Biashara Podcast

    Uzalishaji wa mayai | Uchumi na Biashara Podcast

    Licha ya Shirika la Afya Dunia, WHO kushauri kuwa binadamu anafaa kula mayai 180 kwa mwaka, imebainika kwamba taifa la Kenya halijaafikia kiasi hicho takwimu zikionesha kuwa mayai 36 tu huliwa kwa wastani kulinganishwa na mataifa mengine mfano taifa jirani la Uganda na Afrika Mashariki.
    Hali hii imesababishwa na Wakenya kuzalisha mayai kwa wingi kwa minajili ya kufanya biashara ikilinganishwa na Uganda ambapo huzalishwa vijijini.
    Mwanahabari wetu Martin Ndiema amesema na wafanyabiashara wa mayai kubaini jinsi uzalishaji na ulaji huathiri biashara yao.

    • 10 min
    GMO na hofu kuhusu bei masokoni | Uchumi na Biashara Podcast

    GMO na hofu kuhusu bei masokoni | Uchumi na Biashara Podcast

    Katika Makala Uchumi na Biashara Podcast, mwanahabari wetu wa Kaunti ya Trans Nzoia, Martin Ndiema amesema na wakulima ili kubaini ikiwa wameridhia kupanda mimea iliyoboreshwa kwa njia ya kijenetiki yaani GMO. Wapo ambao wamekumbatia na wengine kuirai serikali kuutafakari upya kuhusu uamuzi huo wa Baraza la Mawaziri wa kupitisha GMO. Aidha, amesema na mtaalamu wa mimea akizamia ubora wa mazao ya mimea ya GMO, soko la kimataifa na usalama wa chakula kwa matumizi ya binadamu.

    • 8 min

Top Podcasts In Arts

Fresh Air
NPR
The Moth
The Moth
99% Invisible
Roman Mars
Fashion People
Audacy | Puck
Snap Judgment Presents: Spooked
Snap Judgment
Fantasy Fangirls
Fantasy Fangirls